Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mazungumzo ya Vienna, yanajadili kuondolewa vikwazo na kadhia ya nyuklia na yanafanyika baina ya Iran wanachama wa kundi la 4+1 linalojumuisha nchi za Russia, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani pamoja na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya.
Press TV imedokezewa kuwa, ujumbe wa Iran huko Vienna umefanya mazungumzo ya kina na jumbe za nchi zinazoshiriki ili kuzihimiza zichunguze mapendekezo ya Tehran na kutoa mapendekezo yao ili mapatano yafikiwe.
Duru mpya ya mazungumzo ya Vienna ilisitishwa Januari 28, 2022, ili kuwezesha jumbe husika kurejea katika miji mikuu kwa ajili ya mashauriano na kuchukuliwa maamuzi ya kisiasa yenye lengo la kufikia makubaliano. Mazungumzo hayo yameanza tena wiki iliyopita na inatazamiwa pande husika zitafikia mapatano katika siku chache zijazo.
342/